Ghana yaichapa Algeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Samoah Gyana akicheka na wavu

Nahodha wa kikosi cha Ghana Asamoah Gyan alifunga bao la pekee na la ushindi katika dakika za mwisho na kufufua matumaini ya Ghana kufuzu katika robo fainali za michuano ya mataifa ya Afrika.

Katika mechi iliokuwa na nafasi chache ,Gyan alipata bao la ushindi katika njia ambayo haikutarajiwa na wengi baada ya kukimbia na kufunga pasi ndefu iliopigwa na mchezaji mwenza Wakasu.

Timu ya Algeria ilikosa nafasi ya wazi wakati Nabil Bentaleb alipowachenga mabeki wa Ghana na kusukuma mkwaju uliotoka nje karibu na eneo la hatari.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Algeria

Mechi hiyo ilionekana kana kwamba itasalia sare ya 0-0 hadi Gyan alipofanya mambo kuwa 1-0.

Mchezaji huyo alikosa mechi ya kwanza ya Ghana dhidi ya Senegal kutokana na ugonjwa wa Malaria.