Arsenal kumsajili Paulista

Haki miliki ya picha b
Image caption Paulista

Kilabu ya Uhispania Villareal imethibtisha makubaliano na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki Gabriel Paulista katika uwanja wa Emirates.

Katika makubaliano hayo Arsenal kwa upande wake itamtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Joel Campbell kwa Villareal.

Bado kuna maelezo machache katika makubaliano hayo ili yaweze kuafikiwa rasmi na yanatarajiwa kutiwa sahihi siku ya jumatatu ,ambapo beki huyo wa Brazil atafanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla ya kuweka sahihi yake na kilabu ya Arsenal.

Mlinzi huyo wa miaka 24 ambaye alijiunga na kilabu hiyo ya La liga mwaka 2013 amekuwa kiungo muhimu wa manuwari hiyo ya manjano na ameweza kuiwakilisha kilabu hiyo mara 50.