Zambia kumenyana na Cape Verde

Image caption Zambia kuchuana na Cape Verde

Zambia itajua iwapo mchezaji wake nyota anayeichezea kilabu ya Southampton Emmanuel Mayuka ambaye anauguza jeraha la mguu alilopata dhidi ya Tunisia atakuwa tayari kucheza dhidi ya Cape Verde.

Kikosi hicho cha Chipolopolo ni sharti kipate ushindi ili kuimarisha matumaini yake ya kufika katika robo fainali nchini Equatorial Guinea.

''Cape Verde ni wazuri na itakuwa mechi ngumu'',alisema kocha Honour Janza.

Kocha wa Cape Verde Rui Aguas amesema kuwa lengo lao kuu ni kufika robo fainali ya mashindano hayo.

Kikosi chake kitahitaji sare pekee kufuzu katika awamu ya robo fainali ikitegemea matokeo ya mechi nyingine katika kundi hilo.

Wakieleka katika mechi ya jumatatu,Tunisia ina pointi 4,Cape verde na Drc Congo 2 na Zambia 1.