Real Madrid yamsajili Silva

Image caption Mchezaji Lucas Silva aliyesajiliwa na Real Madrid

Kilabu ya Real Madrid imemsajili kiungo wa kati Lucas Silva kutoka kilabu ya Cruizero ya Brazil kwa kitita cha pauni millioni 9.7.

Mchezaji huyo wa miaka 21 ambaye alifanyiwa ukaguzi wa matibabu siku ya jumatatu ameweka sahihi ambayo itamuweka katika kilabu hiyo hadi Juni 30 mwaka 2020.

Silva ameiwakilisha Brazil katika soka ya chini ya umri wa miaka 21 na kuisadia kilabu yake kushinda mwaka 2013 na 2014.

Real ilimnunua kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 16 Martin Odegaard mapema wiki hii.