Andy Murray ambwaga Grigor Dimitrov

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andy Murray

Mcheza Tennis maarufu Andy Murray amembwaga Grigor Dimitrov katika kusaka kibali cha kushiriki mashindano ya wazi ya mchezo wa Tennis ya Australia.

Mshindi huyo wa mchezo wa Tennis Uingereza Murry aliibuka mshindi baada ya kujipatia pointi 6-4 6-7 (5-7) 6-3 7-5 ndani ya saa tatu na dakika 32.

Katika seti ya tano ya mchezo huo dalili za ushindin wa Murray zilianza kuonekana na kisha ushindi huo kudhihirika wazi katika michezo mitano ya mwisho.

Kwa ushindi huo sasa Andy Murray anatarajiwa kukwaana na raia wa Austaralia Nick Kyrgios katika mzunguko wake wa nane.

Murray atakuwa akicheka robo fainal ya 16 katika mashindano Grand Slam ikiwa ndiyo hatua ambayo alimtoa Dimitrov katika michuano ya Wimbledon mwakajana.