Swansea:Bony kuwa mchezaji wa ziada City

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wilfried Bonny

Mkurugenzi wa kilabu ya Swansea John van Zweden anaamini kwamba Wilfried Bonny hatotumiwa katika kilabu mpya ya Manchester City kwa kuwa ataorodheshwa kama mchezaji wa ziada.

Bony alitia sahihi mktaba wa dola millioni 25 ili kujiunga na City mapema mwezi huu.

Na huku Van Zweden akikiri kuwa kuondoka kwa mchezaji huyo katika kilabu ya Swansea ni pigo kubwa,anafikiri kwamba mchezaji huyo wa Ivory Coast atakuwa chaguo la pili baada ya Sergio Aguerro katika uwanja wa Etihad.

Alisema:Tutakosa mabao yaliokuwa yakifungwa na Bony kwa wingi.

Lakini kitu kinachoudhi ni kwamba atasalia katika orodha ya wachezaji wa ziada.