Senegal na Algeria kupambana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezaji wa Algeria Islam Slimani

Algeria itamkosa mshambuliaji wake Islam Slimani ambaye alijeruhiwa katika mechi dhidi ya Ghana ambapo timu hiyo ilishindwa na hadi wakati huo hajafanya mazoezi.

Inamaanisha kuwa wachezaji nyota wa timu hiyo Yacine Brahimi na Sofiane Feghouli watalazimika kuonyesha umahiri wao ambao haujaonekana kufiia sasa.

Viongozi wa kundi hilo Senegal wanahitaji sare ya aina yoyote ili kuufuzu katika robo fainali.

Hatahivyo ,kocha Alain Giresse alionya kwamba bado kikosi chake kitaendelea kucheza kufa na kupona katika mechi hiyo ya mwisho.

Hii inamaanisha ugumu wa kundi hili.