Arsenal yamsajili Paulista

Image caption Paulista

Kilabu ya Arsenal nchini Uingereza imemsajili beki Gabriel Paulista kwa kitita cha Yuro millioni 15 huku mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell akijiunga na kilabu ya Villareal kwa mkopo hadi msimu wa joto.

Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 alishiriki kila mechi ya Villa Real na huenda akacheza mechi yake ya kwanza katika uwanja wa Emirates dhidi ya Aston Villa siku ya jumapili.

Paulista ameweka sahihi kandarasi ya miaka minne na nusu katika uwanja wa Emirates na atalipwa mshahara wa pauni 60,000 kwa wiki.