Gareth Bale akataa kwenda Man United.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Gareth Bale

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale amepinga madai kwamba huenda akahamia Manchester United.

Mchezaji huyo wa Wales alikuwa akihusishwa na uhamisho kuelekea Manchester United huku mlinda lango wa Manchester United David De Gea akitarajiwa kuelekea Real Madrid.

''Sioni nikielekea Manchester United '', Bale aliiambia radio ya Cadena SER.

''Ninafurahia kuwa hapa na tunashinda mataji.Nataka kuendelea kufanya hivyo hapa Real Madrid''.

Bale alijiunga na Real Madrid kwa kitita cha pauni millioni 85 mnamo mwezi Septemba mwaka 2013 na kushinda kombe la kilabu bingwa mwaka uliopita.

Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham amekuwa akikosolewa na baadhi ya mashabiki wa Madrid na alizomwa baada ya kukataa kumpa pasi Cristiano Ronaldo katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Espanyol.