Chelsea yakaribia kumsajili Cuadrado

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Juan Cuadrado

Kilabu ya Chelsea inakaribia kuweka sahihi ya kitita cha pauni millioni 23.3 ili kumsajili kiungo wa kati wa timu ya Fiorentina Juan Cuadrado.

Mchezaji huyo wa Colombia amekubali masharti yote ya kujiiunga na Chelsea na sasa kilabu hiyo inamalizia harakati za mwisho za uhamisho huo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Cuadrado akiichezea timu yake ya taifa

Naye mchezaji wa Chelsea Mohammed Salah huenda akaelekea Fiorentina kwa mkopo miongoni mwa makubaliano hayo.

Hatahivyo mchezaji huyo wa Misri hajakubali kuhusu hatua hiyo ya kucheza katika ligi ya Serie A.