Kutolewa Mali, CAF kuangalia upya kanuni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Shirikisho la Soka Africa CAF Issa Hayatou

Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limesema litaupitia upya utaratibu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu baada ya timu kuwa sawa katika hatua ya makundi.

Hapo jana Guinea iliingia robo fainali kwa ushindi wa mezani baada ya kubahitika kwenye bahati nasibu hiyo huku Mali ikifungasha virago baada ya timu zote mbili kumaliza mechi za makundi zikiwa zote zina point tatu na magoli matatu.

Hadi mechi za kundi D katika hatua za makundi zinamalizika hapo juzi, ni Ivory Coast pekee ndio iliyoingia robo fainali baada ya kuifunga Cameroon.

Utarabu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu umekosolewa na wapenzi wa soko kwamba hautendi haki.

Mkurugenzi wa habari wa shirikisho la soka Afrika Junior Binyam amesema pamoja na kwamba walipaswa kusimamia kanuni za mashindano hayo lakini anadhani ipo haja ya kuboresha utaratibu wa kumpata mshindi pindi tukio kama linapotokea.

Amema sio haki timu kurudi nyumbani kama ilivyofanyika kwa Mali.