Murry atinga fainali Australian Open

Image caption Andy Murry

Mwingereza Andy Murry ameshaingia hatua ya fainali baada ya kufunga mpinzani wake Thomas Berdych katika hatua ya nusu fainali.

Sasa Murry atakuwa na mshindi kati ya mtetezi wa mchezo wa tennis duniani kwa upande wa wanaume Stan Wawnrinka na Mcheza tenis namba moja kwa ubora duniani Novak Djokovic ambao leo watakutana katika mchezo nusu fainali.

Mechi ya fainali itachezwa siku ya jumapili.

Naye Serena William atapambana na Maria Sharapova katika mchezo wa fainali kwa upande wa wanawake siku ya jumamosi.