Congo kuchuana na DR Congo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Timu ya Congo

Kikosi cha DR Congo kitamkosa Yousouff Mulumbu aliyekosa mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Tunisia akiwa na jeraha la goti.

Hatahivyo walifuzu baada ya kupata sare tatu na sasa wanajua kwamba ni sharti waimarishe mchezo wao ili waweze kuendelea mbele.

Uzoefu wa kocha Claude LeRoy kama mkufunzi wa timu hiyo mara mbili utaipa maarifa na fursa ya kusonga mbele.

Haki miliki ya picha afp
Image caption Wachezaji wa Congo wakisherehekea ushindi

Itakuwa mechi ya kwanza kati ya timu hizo mbili katika miaka 41 ambapo Congo iliishinda DR Congo 2-1 mjini Alezandria ,Misri.

Na kihistoria nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano mbao si mzuri.

kuna familia nyingi ambazo zimetawanywa na mpaka wa mataifa hayo mawili.mechi hiyo itatangazwa moja kwa moja katika idhaa yako ya BBC redio mwendo wa saa moja.