Arsenal yaisakama Aston Villa 5-0

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud

Arsenal imepanda hadi nafasi ya tano juu ya Tottenham katika ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Aston Villa mabao 5-0.

The Gunners walidhibiti mchezo na kuchukua uongozi baada ya Olivier Giroud Kupata pasi safi kutoka kwa Mesut Ozil.

Santi carzola alipiga chuma cha goli kabla ya mabao ya Mesut Ozil na Theo Walcot kufanya mambo kuwa 3-0.

Giroud alipiga chuma cha goli na kichwa kizuri kabla ya Carzola kufunga bao la Penalti baada ya mshambuliaji chuba Akpom kuangushwa katika eneo la hatari.

Hector Bellerin baadaye alifanya mambo kuwa 5-0 baada ya kusukuma mkwaju kimo cha nyoka.