Chelsea yatoka sare na Mancity darajani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption David Silva

Chelsea iliimarisha uongozi wake wa alama tano katika jedwali la ligi ya Uingereza dhidi ya Manchester City baada ya kutoka sare ya 1-1 na timu hiyo katika uwanja wa stamford bridge.

Loic Remy aliyeanza kutokana na kupigwa marufuku kwa Diego Costa aliiweka kifua mbele Chelsea lakini dakika chache baadaye David Silva alijibu baada ya makosa ya kipa Thibaut Courtois.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Loic Remy

Chelsea ilikuwa na fursa ya kuongeza alama dhidi ya mabingwa wa ligi Manchester City ili kudhibiti uongozi wa ligi hiyo.

Lakini kutolewa kwa mshmbuliaji Remy na kuwekwa kwa Gary Cahil ilikuwa ishara kwamba kocha Jose Mourinho alitosheka na sare hiyo.