Wezi wavamia nyumba ya Di Maria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mchezaji wa Manchester United Ange di Maria ambaye aliepuka jaribio la wizi nyumbani kwake.

Kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria ndio mwathiriwa wa hivi karibuni wa wizi wa kutumia mabavu nyumbani kwake huko Cheshire Uingereza, BBC imegundua.

Baadhi ya wahalifu walijaribu kuvunja mlango wa nyumba yake katika barabara ya Chelford huko Prestbury siku ya jumamosi jioni ,maafisa wa polisi wa Cheshire wamesema.

Hatahivyo mbiu ya mgambo ilipigwa kabla ya wezi hao kuingia ndani ya jumba hilo na kulazimika kutoroka.

Tukio hilo lilitokea baada ya Manchester United kuicharaza Leicester City mabao 3-1 katika uwanja wa Old Trafford.