Tanzania yataja kikosi cha tenisi .

Image caption Kijana akijifua katika viwanja vya Gymkhana

Wachezaji wa tano wa tennis (lawn) wa Tanzania watakao iwakilisha nchi katika michuano michuano ya vijana ya ITF ya Afrika itakayofanyika Tunisia kuanzia Machi 9 mpaka 22.

Kwa mujibu wa viongozi wa chama cha tennis Tanzania (TTA), ushiriki wao utaleta tija katika maendeleo ya mchezo huo nchini.

Tennisi ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi nchini Tanzania na chama cha mchezo huo kimefanikiwa kuwa wenyeji waq michuano mbalimbali ikiwemo ya Afrika ya Mashariki na Kati inayojumuisha nchi mbalimbali za Afrika.

Kwa mujibu wa kocha Majuto Majaliwa, miongoni mwa wachezaji watakaoiwakilisha nchi ni Georgina Kaindoah (yupo Afrika ya Kusini kimasomo na mazoezi) , Emmanuel Mallya, Frank Mernad, Deogratius Ernest na Mandi Furaji (yupo Uingereza kimasomo na mazoezi-.

Michuano hiyon itafanyika katika mji wa Tunis. Nchi mbalimbali za Afrika zitashiriki na kuwakilishwa na wachezaji watano.

Miongoni mwa nchi ambazo tayari zimetaja wachezaji wake ni pamoja na Rwanda, ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari, waliochaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo ni Ernest Habiyambere, Cedric Tuyishimwe, Mutuyimana Chantal, Flavia Kayitesi na Evelyne Kwizera, ambao walifuzu katika michuano iliyofanyika Dar es Salaam, Tanzanua kati ya Januari 10-19.