Ligi daraja la 1 kupata udhamini:TFF

Image caption Wachezaji ligi daraja la kwanza wakimenyana

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko mbioni kupata mdhamini wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Ligi Daraja la Kwanza inashirikisha timu 24 zinazocheza katika makundi mawili ya timu 12 kila moja kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Udhamini huo utakuwa ni kwa msimu wa mwaka 2015/2016

Timu zinazocheza FDL msimu huu ni African Lyon (Dar es Salaam), African Sports (Tanga), Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Faso (Morogoro), Friends Rangers (Dar es Salaam), Geita Gold (Geita), Green Warriors (Dar es Salaam), JKT Kanembwa (Kigoma), JKT Mlale (Ruvuma) na JKT Oljoro (Arusha).

Nyingine ni Kimondo (Mbeya), Kinondoni Municipal Council (Dar es Salaam), Kurugenzi (Iringa), Lipuli (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers (Tabora), Toto Africans (Mwanza), na Villa Squad (Dar es Salaam).

Kupatikana kwa mdhamini ni habari njema kwa TFF katika uendeshaji wa ligi hiyo, ambayo itatoa timu zitakazopanda daraja na kucheza ligi kuu ya Tanzania.