Azam kumaliza ziara DRC leo

Image caption Kikosi cha Azam FC

Timu ya soka ya Azam ya Tanzania leo itamaliza ziara yake nchi Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kucheza mchezo wa mwisho na klabu ya Don Bosco .

Mchezo utapigwa majira ya saa tisa kwa saa Afrika Mashariki itafuatiwa na mechi kati ya Mabingwa wa DRC TP Mazembe dhidi ya Mabingwa wa Zambia Zesco United.

Ziara ya Azam ni maandalizi katika kujiandaa na michuano ya klabu bigwa barani Afrika pamoja na ligi kuu ya Tanzania inayoendelea .

Azam walianza ziara yao kwa kupoteza mchezo mbele ya TP Mazembe kwa kichapo cha bao 1-0.

Kisha wakakubali suluhu ya mabao 2-2 dhidi ya mabigwa wa Zambia katika mchezo wao wa pili.