Ligi kuu Tanzania Bara ni Yanga&Coastal

Yanga yaivaa Coastal Union ili kuiondoa Azam kileleni ligi kuu

Dar es Salaam.

Image caption Raha ya mchezo,shangwe

Baada ya kuwaonya wachezaji wake kutoamini “ndumba” uchawi katika kushinda mechi na badala yake wajitume uwanjani, kocha wa mabingwa wa zamani wa soka Tanzania Bara, Mdachi Hans Pluijm atakuwa na kibarua kingine wakati timu yake itakapocheza na Coastal Union Jumatano jioni katika mechi ya ligi kuu katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Pluijm juzi alisema kuwa hakufurahishwa na sare ya kutofungana dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara inayoshiriki ligi kuu kwa mara kwanza, hivyo kuwataka wachezaji wake kujituma zaidi ili timu iweze kushinda na kushika usukani wa ligi.

Yanga, ambao pia ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF Confederation Cup), ipo nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na alama (points) 19, ikiwa nyuma ya mabingwa watetezi na wawakilishi wan chi katika kombe la vilabu la mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa alama mbili.

Mechi yao dhidi ya Coastal Union ni mkakati wa kuitoa Azam kileleni. Hata hivyo, Yanga isitegemee ushindi rahisi kutoka kwa wapinzani wao, ambao wapo katika nafasi ya saba katika msimamo wakiwa na pointi 17, mbili tu nyuma ya Yanga.

Yanga ilisafiri kwa basi la timu kuelekea mkoa wa Tanga (Kaskazini mwa Tanzania) , umbali unaokadiriwa kuwa karibu kilomita 350 ( wastani wa maili 170)