Ronaldo ana thamani ya pauni milioni 300

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo

Jorge Mendes wakala wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo amesema mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni 300 ikiwa ataamua kuihama klabu yake ya Real Madrid.

Wakala huyo amesema ikiwa timu yake itataka kuuza kwa sababu yoyote ile ni lazima timu inayomtaka itoe kiasi hicho cha fedha.

Ronaldo, mwenye wa miaka 29, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Dunia Mwezi uliopita alikua akihusishwa kurudi katika klabu yake zamani ya Manchester United.

Mendez akasisitiza kuwa nyota huyo atasalia katika timu ya Real Madrid pamoja na kupendwa na mashabiki wa Manchester United.

Wakala huyo aliyewahi kuwa Dj na mmiliki wa Klabu za usiku, ni mwakilishi wa nyota wengine katika soka kama Radamel Falcao, Angel Di Maria, James Rodriguez, David De Gea, Victor Valdes na Diego Costa. Pamoja na makocha Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari.