Timu ya kriketi India yaalikwa Tanzania

Image caption Timu ya wanawake ya mpira wa magongo kutoka India

Timu ya kriketi ya wanawake ya India itakuwa miongoni mwa timu tatu zitakazoshirki michuano ya kombe la wanawake ya T20 itakayochezwa Dar es Salaam Februari 22.

Nchi nyingine zitakuwa ni Kenya na Uganda. Kwa mujibu wa viongozi wa chama cha kriketi Tanzania (TCA), lengo la kuialika India ni kuzipa uzoefu timu za Afrika Mashariki katika mchezo wa kriketi.

India ni moja kati ya nchi za Asia zinazoongoza katika mchezo wa kriketi na kushiriki kombe la dunia mara kwa mara.

Michuano hii itafanyika wakati nchi za Kenya, Uganda, Nigeria, Namibia na Botswana zinatarajiwa kuwasili Tanzania kuanzia Februari 4 kwa ajili ya michuano ya wanaume ya Afrika chini ya miaka 19 Daraja la 1 (Division 1) itakayoanza Jumamosi katika viwanja vya Annadil Burhani, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na Gymkhana Club.