CAF yampiga marufuku refa aliyezua utata

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Refa allipepigwa marufuku

Refa aliyesimamia mechi ya robo fainali kati ya Tunisia na waandalizi wa kombe la Afrika Equitorial Guinea amepigwa marufuku ya miezi sita na shirikisho la soka barani Afrika CAF baada ya kuwapatia Equitorila Guinea penalti katika mazingira ya kutatanisha kabla ya timu hiyo kushinda mechi hiyo 2-1..

Maafisa wa Tunisia walimvamia Rajindraparsad Seechurn,baada ya mechi hiyo kukamilika na shirikisho lao la soka limepigwa faini ya dola 50,000.

CAF pia inataka Tunisia kuomba msamaha kwa kutoa madai kwamba shirikisho hilo linapendelea mataifa kadhaa.

Tunisia pia imeagizwa kulipa faini ya uharibifu wa mlango pamoja na friji katika chumba cha kujiandaa katika uwanja wa Bata.