Jinamizi la maumivu lamuandama woods

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tiger Woods asumbuliwa na maumivu ambayo yanaelezwa kuathiri maendeleo yake kimchezo

Mcheza Gofu Tiger woods ameendelea kuandamwa na tatizo la kuwa majeruhi baada ya kupata maumivu ya mgongo.

Maumivu haya yamesababisha Woods kujitoa katika michuano ya (Farmers Insurance Open) inayoendelea huko Torrey.

Woods mwenye miaka 39 alizungumza na washiriki wenzake kabla ya kuingia kwenye gari na kuondoka.

Hii ilikua ni michuano ya pili kwa mchezaji huyu kushiriki baada ya kufanyiwa upasuaji uliomkosesha kushiriki michuano mingi mwaka jana.