Bony achukua nafasi ya Jovetic

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Stevan Jovetic (kulia) akiwa kwenye mchezo wa ligi kuu England

Man City imemuengua Mshambuliaji Stevan Jovetic katika kikosi kinachoshiriki michuano ya klabu bigwa ulaya na nafasi yake kuchukuliwa na Wilfried Bony.

Kuwepo kwa Bony kulisababisha timu hiyo kuwa na mchezaji mmoja zaidi wa kigeni kuliko wanaruhusiwa katika mashindano ya Ulaya.

Bony alisajiliwa na City mwezi uliopita akitokea Swansea City kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 25.

Uamuzi wa meneja Manuel Pellegrini kumuacha Jovetic unaamaanisha Man City itabaki na washambuliaji watatu wakubwa ambao ni Sergio Aguero Edin Dzeko na Wilfried Bony.

Jovetic, aliyekosa sehemu kubwa ya msimu uliopota sababu ya kuandamwa na majeraha ya nyama za paja amefunga jumla ya mabao 11 toka aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 22 toka Fiorentina mwaka 2013.