Chelsea sasa yaongoza kwa pointi saba

Haki miliki ya picha PA
Image caption kocha mourinho

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kwamba haoni uongozi wa alama 7 juu ya jedwali la ligi ya Uingereza ni fursa ya timu hiyo kushinda ligi hiyo mwaka huu.

The Blues iliishinda Aston Villa 2-1 siku ya jumamosi huku Manchester City Inayoshikilia nafasi ya pili katika jedwali hilo ikiangukia sare ya 1-1 dhidi ya Hull City.

James Milner alifunga bao la Mancity lakini hakuisaidia timu yake kupunguza pengo lililopo kati yake na Chelsea katika uongozi wa Ligi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Manchester city

Hull City ilikuwa ya kwanza kufunga bao kupitia mchezaji David Meyler.

Everton na Liverpool nazo zilitoka sare ya 0-0 katika Merseyside Derby iliochezwa katika uwanja wa Goodison Park

Haya hapa baadhi ya matokeo ya mechi zilizochezwa jumamosi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption liverpool

Tottenham 2 - 1 Arsenal

Aston Villa 1 - 2 Chelsea

Leicester 0 - 1 Crystal Palace

Man City 1 - 1 Hull

QPR 0 - 1 Southampton

Swansea 1 - 1 Sunderland

Everton 0 - 0 Liverpool