Wabuni mbinu kuepuka Vurugu viwanjani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wananchi wakitawanywa nchini Brazil

Klabu ya Soka nchini Brazil imekuja na wazo jipya la kupambana na tatizo la vitendo vya kihuni viwanjani miongoni mwa Mashabiki.

Klabu ya Rucife inayocheza ligi ya juu nchini humo imewafunza Wazazi kadhaa, wakina Mama wa baadhi ya Mashabiki wao hasa mashabiki walio vijana ili waweze kuwazuia Watoto wao kujihusisha na vurugu viwanjani.

Tatizo la Mashabiki kujihusisha na vitendo vya vurugu limekua likikua katika baadhi ya maeneo ya Amerikay a kusini.

Katika tukio linalokumbukwa Mwaka jana , Mshabiki mmoja alipoteza maisha baada ya Sinki la Choo kudondoshwa kutoka juu na Mshabiki mpinzani walipokuwa Uwanjani.