Je Sepp Blatter ataibuka mshindi tena?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Fifa Sepp Blatter

Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa, Sepp Blatter na mahasimu wake kwenye kinyang'anyiro cha Urais wamefaulu jaribio la uadilifu.

Tume ya uchaguzi ya Fifa imewapitisha Sepp blatter na mahasimu wake watatu kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Shirikisho hilo utakaofanyika tarehe 29 mwezi May.

Taarifa ya Fifa imesema wote wanne wanakidhi vigezo vya kuwania Urais.

Rais wa shirikisho la Soka la nchini Uholanzi,Michael Van Praag na wa Jordan Mwana mfalme Ali bin Hussein watasimama kidete dhidi ya Blatter na Winga wa zamani wa timu ya taifa ya Portugal Luis Figo.

Blatter mwenye umri wa miaka 78 amekuwa Rais wa shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na anawania muhula wa Tano.