Viwanja sita kuwaka moto Ligi England

Timu kumi na mbili zitajitupa Uwanja leo kuwania alama tatu muhimu katika ligi kuu ya England Katika uwanja wa Stamford Bridge vinara wa ligi hiyo Chelsea watawakaribisha Everton,huku kiungo Cesc Fabregas akirejea dimbani baada ya kupona majeruhi.

Kwa upande wake kocha wa Everton amesema kipa namba moja Tim Howard atakuwepo golini japo kukiwa na mashaka ya kumkosa mlinzi kisiki Leighton Baines. Manchester United watakua katika uwanja wao wa nyumbani Old Trafford kuwakabili Burnley, united watamkosa Luke Shaw huku wakihitaji kushinda mchezo huu ili kurejea nafasi ya tatu.

Southampton watakipiga na West Ham mchezo utakaopigwa kwenye dimba la St Mary's,

Man city watakua wageni wa Stoke City katika mchezo utakaochezwa Britannia Stadium, City itawakosa Yaya Toure na Wilfried Bony walikua katika michuano ya Afrika. Michezo mingine itazikutanisha West Brom dhidi ya Swansea na Crystal Palace wakiwakabili vijana wa Newcastle United.