JKT MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON

Klabu ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu kwenye mechi.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.

Kamati imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile usajili huo ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi yake ya mwisho ya ligi.