Aston Villa yamtimua Kocha wake

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert

Aston Villa imemtimua kocha wake Paul Lambert baada ya Klabu hiyo kushuka kwenye Msiamo wa ligi kuu England na kuwa hatarini kushuka daraja

Villa ilipoteza mchezo kwa kupigwa Mabao mawili kwa sifuri na Hull city siku ya jumanne, ikiwa ni mechi yao ya 10 bila kuondoka na ushindi

Mskoti huyu aliteuliwa mwaka 2012, na kusaini mkataba ambao utamalizika mwezi June mwaka 2018.

Kocha wa kikosi cha kwanza Scott Marshal na Kocha wa Magolikipa Andy Marshall wanashikilia nafasi ya Lambert kwa sasa