Vilabu vya Manchester vyawika EPL

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Manchester City

Sergio Aguero alifunga bao lake la kwanza tangu mwezi Disemba na kuisadia Manchester City kuimarisha harakati zake za kushinda kwa mara nyengine taji la ligi kuu ya Uingereza baada ya kuichapa Stoke City mabao 4-1.

Mancity ambayo ilikuwa haijawahi kushinda katika uwanja wa Britania katika ligi ya Uingereza ilichukua uongozi kupitia Aguero.

Mshambuliaji wa stoke Peter Crouch alisawazisha kupitia bao lake la kichwa lakini James Milner aliiweka kifua mbele City baada ya kufunga kupitia kichwa.

Baadaye Aguero alifunga bao lake la pili kupitia mkwaju wa Penalti baada ya david Silva kuchezewa visivyo kabla ya Samir Nasri kufunga bao la nne.

Mchezaji wa ziada Chris Smalling alifunga mabao mawili ili kuisaidia manchester United kuishinda Burnley na kupanda hadi nafasi ya tatu katika ligi ya Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Manchester United

United hatahivyo watamkosa Phil Jones na Daley Blind kwa kupata majeraha lakini Smalling aliifungia manchester bao lake la kwanza baada ya pasi safi kutoka kwa Radamel Falcao.

Mchezaji wa Burnly Danny Ings alisawazisha baada ya Kierran Trippiers kutoa krosi safi.

Baadaye Smalling alifunga bao lake la pili baada ya krosi yake Angel Di Maria.

Ings karibia aifungie Burnley bao la pili kabla ya Robin Van Persie kufunga mkwaju wa penalti baada ya Di Maria kuangushwa katika eneo la hatari.