Chelsea,Everton zashutumiwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Chelsea na Everton waligombana uwanjani

FA imezishutumu klabu za Everton na Chelsea baada ya wachezaji wa timu hizo mbili kugombana uwanjani.

Klabu hizo zinashutumiwa kwa kushindwa kuhakikisha kuwa wachezaji wake wanaepuka mivutano uwanjani na kuepuka vitendo vyenye kuchochea vurugu.

Mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic hatachukuliwa hatua zaidi baada ya kugombana na James McCarthy, kwenye mchezo wa jumatano wa ligi kuu ya England ambapo Chelsea iliondoka na ushindi wa goli moja bila dhidi ya Everton.