Aliyefutwa na Tottenham kuifunza Villa

Image caption Tim Sherwood ndiye kocha mpya wa Aston Villa

Tim Sherwood ameteuliwa kama meneja mpya wa kilabu ya Aston Villa baada ya kuweka sahihi ya kandarasi ya hadi mwaka 2018.

Villa ilimfuta kazi Paul Lambert siku ya jumatano baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi kumi ilizocheza ambapo walifunga bao mbili pekee.

Sherwood mwenye umri wa miaka 46 alichukua mahala pake Andrew Villa Boas kama menaja wa Tottenham mnamo mwezi Disemba mwaka 2013 lakini akafutwa kazi mwishoni mwa msimu uliopita na amekuwa bila kazi wakati wote huo.

''Ni heshima kubwa kusimamia moja ya vilabu vikubwa katika soka ya Uingereza alisema Sherwood.''Siwezi kungojea kuanza na niko tayari kukabiliana na changamoto''.

Sherwood ataiongoiza Villa ambayo imeshindwa kuimarika tangu ilipochukua pointi 10 katika mechi zake nne za kwanza na kufunga mabao 12 kati ya mechi 25.