Kolo Toure athibitisha kustaafu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kolo Toure mstaafu

Mlinzi wa timu ya Liverpool Kolo Toure ameuthibitishia ulimwengu kuwa anastaafu kusakata kabumbu la kimataifa akiwa na timu ya nyumbani Ivory Coast,wiki moja baada ya kuwasaidia Tembo hao kutwaa kombe la mataifa ya Afrika .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na tatu sasa, ameeleza wazi kuwa mchezo wake wa mwisho ni dhidi ya timu ya Equatorial Guinea hapo ndo mwisho wake kuonekana viwanjani.

Kolo anasema anaipenda nchi yake na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake ni Kandanda,lakini akatanabaisha hufika wakati asitishe.

Kolo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na chombo kimoja mjini Abidjan, Toure anasema najisikia vibaya sana kuwafahamisha kuwa niwakati wangu kuwaaga. Lengo0 langu lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa, na nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu sana kuufanya.

Toure amekuwa kiungo muhimu sana katika kuutengeneza ushindi wa timu na taifa lake katika kipindi cha miaka ya 2006, 2010 and 2014 akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia..

Ametua katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mara saba ,akiwa amekosa penati mbili katika mechi mbili za fainali dhidi ya Egypt mwaka 2006 na ingine ni ile ya Zambia mwaka 2012 kama unakumbuka vyema.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Koro kazini enzi hizo.

Mchezaji huyo nguli ambaye amesukuma gozi kwa miaka kumi na mitano uwanjani akiwa mchezaji wa kimataifa na anamuacha meneja wa timu yake ya Ivory Coast Herve Renard akiwa na tabasamu tele katika kumtafuta mrithi wa Kolo

Na kolo amemtaja mrithi wake kuwa ni Ousmane Viera Diarrassouba, ambaye atakaba nafasi ya ulinzi baada yake.

Nadai huwa hafanyi makosa pindi afanyapo uchaguzi wa nani akae wapi, naamini mrithi wangu atawapika vyema vijana wawili Eric Bailly na Wilfried Kanon.na hivyo anaamini Viera atamuwakilisha vyema.

Kolo alianza kuonesha cheche zake katika timu ya ASEC Mimosas ya Abidjan, Toure kisha akaelekeza daluga zake kwenye timu ya Arsenal mnamo mwaka 2002 na alikuwa chachu ya kutofungwa kwa msimu wa miaka miwili mfululizo nazungumzia miaka ya 2003/4.

Lakini baadaye alimwaga wino katika kilabu cha Manchester City mnamo mwaka 2009 kabla hajaelekea katika timu ya Liverpool kwa uhamisho wa bure msimu uliopita.