Kenya yaifunga Burundi wavu ufukweni Tanzania

Image caption Mpira wa mchangani

Kenya (wanaume) imeifunga Burundi kwa seti 2-1 katika michuamo ya wavu ya ufukweni ya Kanda ya 5 kwa ajili ya

kufuzu kucheza michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani mjini Rio de Janeiro, Brazil.

katika michuano inayoendelea katika fukwe za Mbalamwezi jijini Dar es Salaam, Kenyawaliwatala seti ya kwanza na kushinda 21-13.

Burundi, katika jitihada za kupata ushindi, walifanikiwa kushinda seti ya pili kwa pointi 21-14. Seti ya tatu

ilikuwa na ushindani na Kenya walifanikiwa kupata pointi 15 dhidi ya 13 za wapinzani wao.

Katika mechi nyingine ya wanawake, Burundi walishinda kwa seti 2-1 Mechi kadha zinaendelea Jumatano huku

wenyeji Tanzania wakicheza na Kenyakatika upande wa wanaume.

Kenya (wanawake) watacheza na Tanzania. Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa wenyeji wa michuano ya kufuzu kucheza

Olimpiki.Timu zinazoshiriki michuano hiyo ya Dar es Salaam ni Kenya, Burundi na Tanzania.

Timu zitakazoibukwa washindi kwa upande wa wanaume na wanawake zitashiriki katika michuano ya Afrika itakayofanyika Congo Brazzavile, hatua ya mwisho kabla

kuelekea Rio de Janeiro.