Houston Dash yamsajili Stephanie Roche

Image caption Puskas Stephanie akifurahia ushindi

Mshindi wa tuzo ya Puskas Stephanie Roche amesajiliwa na timu ya Houston Dash inayoshiriki liogi ya wanawake ya Marekani.

Mshambuliaji huyu amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo.

" Nina matumaini ya kuendelea na kufanya vizuri katika timu hii," alielezea mchezaji huyo.

Mshambuliaji huyo aliteuliwa kuwania tuzo ya goli bora la mwaka na shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa.

Roche alianza kuichezea timu ya taifa ya jamuhuri ya Ireland akiwa na miaka 14.