Mayweather akubali kuzichapa na Pacquiao

Haki miliki ya picha AP
Image caption Floyd Mayweather kuzichapa na Manny Paicqiao mwezi Mei 2

Mwanamasumbwi raia wa Marekani Floyd Mayweather Junior ametangaza kuwa pigano lililosubiriwa kwa siku nyingi na mwanamasumbwi raia wa ufilipino Manny Pacquiao litafanyika mjini Las Vegas tarehe mbili mwezi Mei mwaka huu

Pambano hilo kati ya mabingwa hao wa unazi wa welterweight limekuwa likisubiriwa kwa miaka mitano.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mayweather

Baada ya mazungmzo ya muda mrefu hatimaye kandarasi imetiwa sahihi.

Pigano hilo litakuwa la gharama kubwa zaidi ya historia ya dola milioni 250.

Wawili hao wanatajwa kuwa bora zaidi katika ndondi za uzani huo duniani.