Yanga yamuacha Coutinho kwenda Botswana

Image caption Coutinho

Baada ya Azam FC kukwea pipa ( kupanda ndege) mapema wiki hii kuelekea Khartoum, nchini Sudan kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Yanga inaondoka Jumatano kuelekea Gaborone, Botswana, huku kukiwa na habari ya kuachwa kwa kiungo mkabaji, Mbrazil Andrey Coutinho.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema Coutinho, Mbrazil pekee aliyebaki Yanga baada ya Wabrazil wengine, akiwemo aliyekuwa kocha mkuu, Marcio Maximo kutupiwa virago kwa utendaji usioridhisha, amepata majeraha katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Tanzania Bara na kuna asilimia kubwa yay eye kutosafiri. Amekuwa kifanya vizuri sana katika mechi za hivi karibuni.

Msafara wa Yanga unategemewa kuwa na wachezaji 20. Mechi ya marudiano itafanyika Ijumaa na mabingwa hao wa zamani Tanzania Bara wanategemewa kurudi nyumbani wikiendi.

Yanga ilishinda 2-0 katika mechi ya kwanza na inahitaji ushidni au sare ya aina yoyote kusonga hatua inayofuata.