Fernando Alonso: atoka hospitalini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari ya mashindano ya Mclaren

dereva wa timu ya Mclaren fernando alonso ametoka hospitali kufuatia kupata ajali.

Bigwa huyu wa dunia mara mbili amerudi nchini Hispania kujiunga na familia yake kwa ajili ya mapumziko na kuweza kupona kabisa.

Majeruhi haya ya Alonso yatasabaisha kukosa kwa raundi ya tatu ya majaribio ya magari yatakayofanyika kuanzia Alhamis huko Barcelona.

Timu ya Mclaren imesema madereva Kevin Magnussen atashirikiana na Jenson Button katika kujaribu magari.

Timu za magari yaendayo kasi zinajiandaa kuanza msimu mpya utakaoanza Machi 15.