Andy Murray atinga nane bora

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray

Mcheza tenesi Andy Murray ameinguia hatua ya nane bora katika michezo ya tenesi ya Dubai,Murray amemfunga Joao Sousa wa Ureno kwa seti 6-0 6-2.

Sousa, ambae hajawahi kushinda seti yoyote katika mi8chezo mitano iliyopita aliyokutana na Murray anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora duniani.

Nyota huyu wa tenesi alipata ushindi wa seti ya kwanza kwa dakika 21 na kumalizia seti ya pili iliyopleke Sousa kushindwa kurudisha.

Murray atachuana na mshindi kati ya Marcos Baghdatis au Borna Coric wa Croatia