Wenger:Presha ya ushindi hainisumbui

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkunfunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Presha ya Arsenal kuwa chaguo la wengi katika kufuzu robo fainali ya kombe la vilabu bingwa barani ulaya dhidi ya Monaco inaeleweka amesema mkufunzi wa kilabu hiyo Arsene Wenger.

Kilabu hiyo ya London imekuwa ikiyaaga mashindano hayo katika misimu minne iliopita.

''Ufaransa wanaweza kutuvisha taji la kuwa bora dhidi ya Monaco lakini hainisumbui mimi'',amesema Wenger wakati ambapo anatarajia kuingoza kilabu yake katika mechi dhid ya Monaco leo usiku katika uwanja wa nyumbani wa Emirates.

Nafurahi kwamba Monaco imerejea katika ulingo wa vilabu vikubwa baada ya kuwa katika ligi ya daraja la pili.

''Ilikuwa mara yangu ya kwanza katika kilabu kubwa lakini sasa mimi ni meneja wa Arsenal kwa miaka 18 na sasa ninajitayarisha kupambana na Monaco''.alisema Wenger.