Will Stevens: dereva wa kwanza Manor

Haki miliki ya picha Getty

Timu ya magari yaendayo kasi ya Manor ya fomula 1, imemtangaza Will Stevens kuwa dereva wa timu hiyo.

Stevens atakua dereva wa timu ya kwanza katika msimu mpya wa mbio za magari yaendayo kasi.

Manor, bado hawajatangaza nani atakua dereva wa pili w timu hiyo anayojiandaa kushiriki michuano ya magari itayofanyika Melbourne, Australia kuanzia 15 Machi.

Timu hiyo ilikua ikifahamika kama Marussia kabla ya kubadilishwa na kuitwa Manor kwa sababu za kibiashara .

Japo kuwa hawajasema kama wanampango wa kubadilisha nembo yao au kubadilisha aina ya muundo wa magari yaliyotumika msimu uliopita .