Arsenal hoi dhidi ya Monaco UEFA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Arsenal

Matumaini ya Arsenal kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo imeingia nyongo hapo jana baada ya kubali kipigo nyumbani mbele ya mashabiki wao kutoka kwa Monaco ya Ufaransa cha mabao matatu kwa moja.

Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Dimitar Berbatov ambaye naye alirejea England alikuwa ni miongoni mwa waliopachika magoli hayo kwa upande wa Monaco.

Huku magoli mengine yakipachikwa na Geoffrey Kondogbia na Yannick Ferreira Carrasco.

Goli la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Oxlade Chamberlain.

Katika mechi nyingine ya michuano hiyo Bayer Leverkusen ya Ujerumani ilipata ushindi wa bao kwa 0 dhidi ya Atletico Madrid. Goli hilo pekee la Bayern Liverkusen lilitiwa kimiani na Hakan Calhanoglu