Henry aimezea mate kazi ya Arsene Wenger

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Thiery Henry

Mchezaji mkongwe wa Arsenal Thierry Henry amefichua kuwa ndoto yake kuu ni kumrithi Mkufunzi Arsene Wenger katika kilabu ya Arsenal.

Mchezaji huyo wa zamani ambaye ndio anayeongoza kwa idadi ya mabao katika kilabu hiyo akiwa na magoli 228 aliripotiwa kupewa fursa ya kuanza kufunza soka katika chuo cha ukufunzi wa soka katika kilabu hiyo mapema mwezi huu.

Raia huyo wa Ufaransa amekiri kwamba ana mipango ya kumrithi Wenger wakati kocha huyo atakapoamua kustaafu.

Akizungumza wakati wa maonyesho ya Jonathan Ross Show,Henry alisema:

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsene Wenger

''Sijui ni kwa mda gani Wenger anataka kusalia kama mkufunzi wa Arsenal.

Lakini ni sharti niwe na uzoefu wa kutosha kuchukua wadhfa huo.

Kuwa Mkufunzi wa Arsenal ni ndoto yangu kubwa ,lakini nafaa kujifunza mwanzo ,hicho ndicho kitu muhimu''.