Ligi kuuTanzania Bara kuanza Jumatano

Image caption Timu ya Mtibwa Sukari

Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi katika viwanja vitatu tofauti siku ya Jumatano.

Mkoani Morogoro katika uwanja wa Manungu-Turiani , wenyeji timu ya Mtibwa Sugar (wakiwa na pointi 19)watawakaribisha majirani zao, timu ya Polisi Morogoro.(nao wakiwa na pointi 19).

Katika uwanja wa Azam Complex – Chamazi, uliopo kando kidogo ya Dar es Salaam, maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha maafande wenzao timu ya Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya, huku timu ya Ruvu Shooting wakiwa katika Uwanja wa nyumbani Mabatini – Mlandizi, mkoa wa Pwani kuwakaribisha timu ya Ndanda FC.

Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 31, huku mabingwa watetezi, Azam Fc wakifuatia wakiwa na pointi 27