Refa mechi ya Zesco na AS ni Mtanzania

Image caption Nkongo wa nne kutoka kushoto

Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Israel Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi ya AS Kaloum ya Guinea.

Katika mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika kibendera John Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri Sheha wote kutoka Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin Shishana kutoka nchini Afrika Kusini

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 13,14,15 Machi mwaka huu nchini Zambia.