FA:Cisse na Evans kutocheza mechi 7

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji Papis Cisse wa Newcastle na Jonny Evans wakitemeana mate.wawili hao wamepigwa marufuku ya mechi 7 kila mmoja huku Cisse akiongezwa marufuku ya mechi moja.

Shirikisho la Soka nchini Uingereza FA limewapiga marufuku wachezaji Jonny Evans wa Manchester United na Papiss Cisse wa Newcastle kutocheza mechi saba kwa kutemeana mate.

Evans mwenye umri wa miaka 27 alikuwa amekana mashtaka ya kumtemea mate Cisse katika mechi dhidi ya Manchester ambapo kilabu hiyo ya Old Trafford iliibuka mshindi kwa 1-0.

Haki miliki ya picha press association
Image caption cisse na evans

Bwana Evans alipinga madai hayo lakini yakabainishwa,ilisema taarifa ya FA.

Cisse mwenye umri wa miaka 29 alikubali mashtaka aliyowekewa na sasa amepigwa marufuku kwa mechi nane kwa kuwa tayari alikuwa amehudumia marufuku msimu huu.