Shirikisho la mbio za Biaskeli lawamani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lance Armstrong

Shirikisho la Mbio za baiskeli duniani limelaumiwa kwa kufumbia macho tatizo la kutumia dawa zilizopigwa marufuku za kusisimua misuli michezoni.

Baada ya mwaka mmoja wa uchunguzi ulifanywa na tume iliyoundwa imesema katika miaka ya 1990 katika karne hii shirikisho hilo lilifumbia macho marufuku ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

Shirikisho hilo limetupiwa lawama kuwa lilishindwa kutumia kanuni zake ipasavyo. Pia limelaumiwa jinsi lilivyoshughulikia suala la mwendesha baiskeli raia wa Marekani Lance Armstrong kwa madai kwamba alipewa upendeleo japo baadae alifungiwa moja kwa moja kushiriki michuano ya baiskeli