India kidedea kombe la dunia kriketi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption India imeichapa Ireland Wiketi nane

Timu ya kriketi ya India imeibanjua timu ya Ireland kwa jumla wiketi nane kwenye michezo ya kombe la dunia la kriketi.

Ushindi huo wa india ulichagiwa kwa kufanya vizur kwa wachezaji wake wakiongozwa na Shikhar Dhawan aliepata mitupo (100) na Rohit Sharma aliepata (64).

Matumaini ya Ireland kufuzu hatua ya nusu fainali imekua ngumu baada ya kupoteza mchezo huo kwa kundi B,wakishika nafasi ya nne kwa alama 6.

India wanaongoza kundi B wakiwa na alama 10 baada ya kucheza michezo mitano ya michuano wakiwa wameshinda yote.